WAZIRI MCHENGERWA ATOA SIKU 14 KWA COSOTA KUKAMILISHA MAREKEBISHO YA SHERIA.
Na John Mapepele
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa ameiagiza Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) kukamilisha marekebisho ya Sheria ya Hakimiliki pamoja na Kanuni kabla ya tarehe 01/11/2022 na kufanya operesheni ya uharamia.
Mheshimiwa Mchengerwa ametoa agizo hilo leo Oktoba 18,2022 Jijini Dar es Salaam katika kikao chake na viongozi wa Kampuni ya Multichoice Tanzania na Azam Media Ltd kufuatia malalamiko ya Kampuni hizo ya wizi wa maudhui.
"Suala la uharamia nafahamu kuwa limekithiri Ofisi ya Hakimiliki toeni elimu kwa wadau na toeni matamko ya kukemea uharamia,"alisema Mhe.Mchengerwa.
Akiendelea kuzungumza katika kikao hicho Waziri huyo alisisitiza kuunda Kamati ya uharamia hivi karibuni ambayo itathibiti uharamia.
Naye Muwakilishi wa Msimamizi wa Ofisi ya Hakimiliki Tanzania Bw.Baraka Katemba alifafanua kuwa tayari Ofisi hiyo imekwisha fanya andaa Kanuni hizo ambazo kama ilivyoelekezwa na Maboresho ya Sheria yanaendelea kufanyiwa kazi na ameahidi kuwa maelekezo yote yaliyotolewa yatakamika kwa wakati.
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Multichoice Tanzania alieleza namna Kampuni hiyo inapata hasara kutokana na Uharamia wa maudhui wanayozalisha kutokana na baadhi ya kurasha maudhui hayo bila kibali chao na pia alieleza namna serikali inakosa mapato kutokana na baadhi ya wadau kutumia ving'amuzi ambavyo wanaviingiza kimagendo na kuvitumia kurusha matangazo.




Comments
Post a Comment