Posts

Showing posts from January, 2023

Mhe. Mchengerwa- Serikali yadhamiria kujenga Chuo Kikuu cha Kiswahili.

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Mohamed Mchengerwa amesema Serikali imedhamiria kujenga Chuo Kikuu cha Kiswahili ili kukuza na kubidhaisha  lugha hii adhimu duniani. Mhe. Mchengerwa amesema haya leo, Januari 25, 2023 jijini Dar es Salaam wakati akimkaribisha   Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa kuhutubia kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo ya Kiswahili. Amesema, hivi sasa Kiswahili ni miongoni mwa lugha zinazokua na kuenea kwa kasi kubwa ulimwenguni ambapo Kiswahili ni miongoni mwa lugha kubwa kumi duniani. Hivyo, kasi ya ufunzaji na ujifunzaji wa lugha hii imekuwa ikiongezeka kila uchao. Aidha,  amesema Kiswahili ni lugha ya mawasiliano mapana katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na kwa upande wa Tanzania licha ya kuwa lugha ya Taifa ndiyo lugha kuu ya mawasiliano. Amefafanua kuwa  lugha ya  Kiswahili kwa sasa imevuka mawanda ya kuielezea lugha yenyewe na hivyo inatumika kuelezea taaluma mbalimbali kama vile afya,...

Mhe. Mchengerwa atatua mgogoro wa mwekezaji na wananchi, wananchi wampongeza Rais Samia.

Image
  Na John Mapepele Wananchi wa eneo la Nyanda  na Utunge wilayani Rufiji wamemshukuru Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mbunge wa Rufiji na MNEC wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Mohamed Mchengerwa kwa kutatua mgogoro wa muda mrefu baina ya mwekezaji wa mradi wa uzalishaji wa sukari na wananchi wa maeneo hayo. Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa wananchi na Mhe. Mchengerwa leo, Januari 22,2023 kwenye eneo la Nyanda, Mwenyekiti Mstaafu wa Kijiji hicho, Amir Omary Magulu amempongeza Mhe. Mchengerwa kwa busara na  jitihada  zake  za kuumaliza  mgogoro huo ambao ulikuwa sugu kwa muda mrefu sasa. Amesema mgogoro huo baina ya mwekezaji huyo ambaye ni Lake Agro  unatokana na ukiukwaji wa makubaliano ya awali  ya  kupewa eneo la uwekezaji na  kutopata taarifa sahihi za uwekezaji. Akitoa suluhisho la mgogoro hilo, Mhe. Mchengerwa ameuomba uongozi wa Wilaya na Halmashauri ya Rufiji kuja kwa wananchi  pamoja na mwekezaji ili kujadili...