Posts

Showing posts from August, 2022

Waziri Mchengerwa atoa wito kwa jeshi kuwa na timu ya soka.

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa ametoa wito  kwa majeshi kuanzisha  timu  ya soka itakayoshiriki ligi kuu nchini ili kuongeza ushindani na mvuto wa ligi. Mhe. Mchengerwa ametoa wito huo usiku wa kuamkia leo Agosti 28, 2022 kwa Mkuu wa Majeshi, Jenerali Jakob John Mkunda katika uwanja wa Gofu wa jeshi wa Lugalo jijini Dar es Salaam wakati akifunga  mashindano ya Gofu ya NBC Lugalo Patron Trophy 2022. Amefafanua kuwa majeshi yamekuwa na historia ya kutoa mchango mkubwa ambapo ameelezea kwamba   wachezaji wengi wanaoshinda katika mashindano mengi wanatoka kwenye majeshi. Aidha amesema kutokana na nidhamu iliyojengeka kwenye majeshi anaimani kuwa jeshi linauwezo wa kuanzisha timu hiyo ambayo itakuwa miongoni mwa timu tishio ndani na nje ya nchi yetu. Amesifu juhudi zinafanywa na jeshi katika kuanzisha klabu ya gofu na  miundombinu ya michezo huo Dar es Salaam na Dodoma na kuruhusu raia kutumia ambapo a...

Dunia yaitazama Royal Tour kupitia mhadhara wa Gurudev

Image
  Na John Mapepele Mamilioni ya watu usiku wa kuamkia leo Agosti 26, 2022 wameitazama  Tanzania  kupitia Filamu ya Royal Tour katika mhadhara maalum uliofanywa na balozi wa amani duniani Gurudev Sri Sri Ravishankar. Gurudev anasakikika  kuwa na wafuasi zaidi ya milioni mia tano duniani kote ambao   humfuatilia  Kila anapotembea dunia kote kuhubiri amani, furaha na upendo. Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo. Mhe. Mohamed Mchengerwa ndiyo aliyewaongoza watanzania  kushiriki kwenye mhadhara huo uliyofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha  Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiambapana na Katibu Mkuu wa wizara yake Dkt Hassan Abbasi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Royal Tour. Katika ukumbi huo ambao ulifurika kwa mamia ya watu na wengi kukosa mahali pa kuketi Filamu hiyo ilichezwa na kuonesha vivutio mbalimbali vya Tanzania ambapo hatimaye ilishangiliwa sana  huku timu ya vyombo vya ndani na nje vilivyoongozana na Mhubiri h...

Mhe. Mchengerwa awaongoza watanzania kumpokea Gurudev Sri Sri Ravishankar

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa leo Agosti 25, 2022 amewaongoza watanzania  kumpokea  kiongozi  mashuhuri duniani ambaye ni kiongozi wa kiroho na balozi wa amani duniani Gurudev Sri Sri Ravishankar. Mara baada ya  kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar es Salaam amepokewa na Mhe  Mchengerwa na Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamagi ya Royal Tour.  Baada ya kuwasili Gurudev Sri Sri Ravishankar amesema amejisikia furaha kuja Tanzania kwa kuwa nchi ya amani. Kiongozi huyo mwenye zaidi ya wafuasi milioni 500 atakuwa na ziara ya siku tatu nchini na anatarajiwa kufanya  tukio la kiutamaduni kukutana na viongozi na kutembelea maeneo ya utalii. Aidha leo jioni majira ya saa 12 atashiriki tukio la kihistoria la  utamaduni wa India na Tanzania na kutoa mhadhara katika   Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Pia...

Waziri Mkuu Achangisha Bilioni 1.2 Serengeti Girls, Tembo Warriors, Asifu Ubunifu wa Wizara ya Michezo

Image
  Na John Mapepele. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa leo Agosti 24, 2022 amechangisha zaidi ya bilioni 1.2 kwa ajili ya kuchangia timu za Serengeti Girls na Tembo Warriors. Harambee hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kutaka timu hizo zichangiwe na wadau baada ya kufuzu kuingia kwenye mashindano ya Duniani. Akizungumza mara baada ya  zoezi hilo, lililofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam ameipongeza Wizara  ya Utamaduni Sanaa na Michezo kwa ubunifu, usimamizi na kutangaza shughuli za michezo kimkakati. Aidha, amewapongeza wadau  wote waliochangia ambapo amesema wameonesha uzalendo wa hali ya juu na kuwa sehemu ya kuzifanya timu hizo kushinda  kwenye mashindano hayo. Katika  tukio hilo  mbali na kupatikana kwa ahadi ya fedha hizo, wadau wameweza kutoa tiketi za wachezaji  kwenda kwenye ma...

Waziri Mkuu Achangisha Bilioni 1.2 Serengeti Girls, Tembo Warriors, Asifu Ubunifu wa Wizara ya Michezo

Image
  Na John Mapepele. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa leo Agosti 24, 2022 amechangisha zaidi ya bilioni 1.2 kwa ajili ya kuchangia timu za Serengeti Girls na Tembo Warriors. Harambee hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kutaka timu hizo zichangiwe na wadau baada ya kufuzu kuingia kwenye mashindano ya Duniani. Akizungumza mara baada ya  zoezi hilo, lililofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam ameipongeza Wizara  ya Utamaduni Sanaa na Michezo kwa ubunifu, usimamizi na kutangaza shughuli za michezo kimkakati. Aidha, amewapongeza wadau  wote waliochangia ambapo amesema wameonesha uzalendo wa hali ya juu na kuwa sehemu ya kuzifanya timu hizo kushinda  kwenye mashindano hayo. Katika  tukio hilo  mbali na kupatikana kwa ahadi ya fedha hizo, wadau wameweza kutoa tiketi za wachezaji  kwenda kwenye ma...

Mhe. Mchengerwa ahesabiwa, asisitiza watu wote kuhesabiwa

Image
  Na John Mapepele, Rufiji . Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa ametoa wito kwa wanamichezo na wasanii wote kujitokeza kuhesabiwa  ili Serikali iweze  kupanga mipango ya maendeleo. Akiongea mara baada ya kuhesabiwa leo, Agosti 23, 2022 kwenye makazi yake Ikwiriri - Rufiji  amesema mafanikio ya kizazi cha kesho yatatokana na kujua idadi sahihi ya takwimu  za sasa. "Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa zoezi hili la sensa kwa kuwa  linalokwenda kutusaidia sana kuleta maendeleo" ameingeza Mhe. Mchengerwa Aidha, amesema sensa  ya mwaka huu ni muhimu  katika sekta za michezo, na sanaa kwa kuwa itasaidia  kupanga namna bora ya kuwahudumia watanzania kwenye sekta hizo. Amesema hiyo itasaidia kupanga namna na kujenga miundombinu  ya michezo kama vile viwanja vya michezo na  arena  za michezo. Amefafanua kuwa sensa itasaidia  mipango ya kibajeti kuandaa kanzi d...

Misri kujenga viwanja changamani Dar, Dodoma, Mwanza na Arusha, yaahidi kutoa mafunzo maalum kwa waamuzi, makocha.

Image
  Na John Mapepele Serikali ya Misri na Tanzania zimekubaliana kuimarisha mahusiano na mashirikiano kwenye  sekta ya  michezo kwa kujenga  miundombinu ya  michezo nchini na  kubadilishana  utaalam kwenye  michezo kwa faida ya pande zote mbili. Hayo yamesemwa leo Agosti 18, 2022 na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa baada ya mkutano wa kujadili mambo mbalimbali ya kuimarisha michezo baina yake na Balozi wa Misri nchini Mhe. Mohamed Gaber Abulwafa. Amesema Serikali ya Misri imekubali kujenga viwanja changamani vya michezo kwenye miji ya Dar es Salaam, Dodoma, Arusha na Mwanza kwa gharama zao ambapo amesema viwanja hivyo vitakuwa vya kisasa ambavyo vitasaidia pia katika mashindano ya kimataifa. Ameongeza kuwa mbali na kujenga viwanja vya michezo Serikali ya Misri imekubali kuisaidia Tanzania kwenye eneo la kutoa mafunzo kwa makocha na waamuzi wa soka ili wawe na viwango ambavyo vinakidhi   matakwa  ya Shirik...

Mhe. Mchengerwa awakabidhi Bendera Taifa Queens, awataka wafuzu Kombe la Dunia.

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa amewakabidhi Bendera yaTaifa timu ya Taifa ya Netiboli ya Taifa Queens kama ishara ya kuwaaga kwenda kwenye mashindano ya kufuzu kushiriki Kombe la dunia yanayofanyika nchini Afrika Kusini. Akikabidhi bendera hiyo leo Agosti 18, 2022 jijini Dar es Salaam, Mhe. Mchengerwa amewataka   kutanguliza uzalendo na utaifa katika mashindano hayo ili kufanya vizuri na hatimaye kufuzu kuingia kwenye mashindano ya dunia.  “Naomba niwaambie ndugu zangu nnyie mnaweza kabisa kuandika historia ya kuwa timu ya tano katika nchi yetu kuingia kwenye mashindano ya dunia endapo mtakuwa wazalendo, nendeni mkacheze kufa na kupona kama ni kuvunjika mkavunjikie uwanjani lakini mrudi na ushindi nyumbani, nasi tutawapokea kwa heshima kubwa” Amefafanua Mhe. Mchengerwa. Aidha, amewataka watambue kuwa wakifanya vizuri watakuwa wamefungua ukurasa mpya wa maisha yao kwa kuwa timu kubwa duniani zitawanunua kitu ambacho k...

Tanzania na Falme za Kiarabu waja na tamasha kubwa la Utamaduni

Image
  Na John Mapepele Tanzania kwa kushirikiana na  nchi zote za falme za kiarabu inatarajia kufanya  tamasha kubwa la Utamaduni Februari mwakani jijini Dar es Salaam. Hayo yamesemwa na leo Agosti 18, 2022 na  Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa baada ya kumaliza mazungumzo na Balozi wa Qatar nchi, Mhe. Husain Ahmad Al- Homaid aliyeambatana na ujumbe kutoka nchini Kuwait. Aidha, amefafanua kuwa nchi hizo kabla ya uamuzi huo walitafiti na kuona kuwa  Tanzania imebarikiwa kuwa na Utamaduni tofauti na nchi nyingi duniani, hivyo kufanya tamasha hilo la pamoja litakuwa na faida kubwa kwa pande zote mbili. Amesema maonesho  hayo ni maalum ya kiutamaduni ambapo yatajikita katika Sanaa za uchoraji, uchongaji pamoja na nyimbo. Ameongeza kuwa Utamaduni na sanaa za Tanzania zina historia ndefu katika ukombozi wa Bara la Afrika ambapo amesisitiza kuwa Baba wa taifa wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere aliwaunganisha watanzania hadi kupata uhuru k...

Waziri Mchengerwa aelekeza vilabu vyote kumiliki viwanja vyake vyenyewe, Yanga na Simba vyaahidi kutekeleza agizo hilo ndani ya miezi sita.

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Agosti 17, 2022 ameelekeza vilabu vyote kumiliki viwanja vyake vyenyewe ambapo timu ya  Yanga na Simba zimeahidi kutekeleza agizo hilo ndani ya miezi sita.  Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo  alipokutana na  watendaji wakuu wa vilabu vinavyoshiriki ligi kuu  jijini Dar es Salaam na  kujadili  namna bora ya kuendesha ligi   kwa ubunifu na ushindani wa hali ya juu ili kuifanya ligi iwe na mvuto. Mhe. Mchengerwa amesema mpango wa vilabu kumiliki  viwanja vyao  ni takwa la kisheri kulingana na Sera ya Michezo nchini. Aidha, Mhe. Mchengerwa amefafanua kuwa  pamoja na mambo mengine kikao hicho kimejadili masuala ya kuzingatia  weledi, nidhamu na maadili. Amesema kwa sasa Serikali haiwezi kukubaliana na vitendo vyovyote vya rushwa na upendeleo katika michezo kwa kuwa vinasaidia kuua na kudidimiza michezo. Amesema dhamira ya Serikali  kwa ...