Posts

Showing posts from June, 2022

Burundi watua Dar kushiriki tamasha la kitaifa la Utamaduni.

Image
  Na John Mapepele Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Maji na Madini nchini Burundi  ndugu Selemani  Khamissi ambaye pia ni mmiliki wa  kikundi maarufu cha taarabu nchini  humo cha Alwatan  kinachoshiriki kwenye Tamasha la Kitaifa  la Utamaduni ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuandaa   tamasha hilo huku akisisitiza kuwa tamasha hilo litaitangaza  vema Tanzania duniani. Akiongea na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na michezo. Saidi Yakubu ofisini kwake jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili amesema Serikali ya Burundi inaunga mkono jitihada za serikali ya Tanzania katika  kuenzi na kuendeleza  utamaduni ndiyo maana  wasanii kutoka Burundi wanashiriki  katika tamasha hili. “Naomba nisema nimefurahi kuja Tanzania kushiriki kwenye tamasha tunawahidi watanzania wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya kuja kuona uzoefu wetu kwenye taarabu kwa kuwa Burundi ina hazina kubwa ya magwiji wa taarabu kutoka miaka...

MHE. MAJALIWA MGENI RASMI TAMASHA LA UTAMADUNI

Image
  Na John Mapepele Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Maadhimisho ya Tamasha la kwanza la kihistoria la Utamaduni  kitaifa  Julai 2, 2022  Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania aliyoyatoa kwenye Tamasha la Utamaduni la Mkoa wa Kilimanjaro la kutaka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuandaa tamasha kubwa la kitaifa la utamaduni litakaloshirikisha mikoa yote ya Tanzania ili kutangaza hazina ya utamaduni wa makabila ya Tanzania Duniani. Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa,  amefafanua kuwa tamasha hilo litaambatana na matembezi maalum ya kitamaduni (Utamaduni Carnival) katika jiji la Dar es Salaam ambayo yameandaliwa njia  maalum za kupita ikiwemo daraja la juu la Mfugale, Kijazi, Tanzanite na daraja la mwalimu Nyerere. Amesema,  tamasha hilo litatoa fursa kwa  ma...

WAZIRI MCHENGERWA: TUZO ZA BET NI NGUZO KUBORESHA SANAA TZ

Image
  Na Mwandishi Wetu, LA, Marekani Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohammed Mchengerwa, amesema watazitumia tuzo za BET za mwaka 2022 kuona maeneo ya kuboresha zaidi katika usimamizi wa sekta ya sanaa nchini Tanzania.  Waziri Mchengerwa ameyasema hayo baada ya kushuhudia Tuzo za BET za mwaka huu 2022 mjini Los Angeles, California, usiku wa kuamkia leo. “Tumeshuhudia tuzo hizi ikiwa pia ni maandalizi ya sisi kuandaa tuzo kubwa kwa upande wa Afrika za MTV, ambapo sehemu ya waandaaji wake ni hawa hawa wa tuzo za BET na kuna maeneo ya kisera na kimageuzi tu tutaendelea nayo baada ya hapo,” alisema Waziri Mchengerwa. Awali, Waziri Mchengerwa alikutana na Makamu wa Rais wa Paramount Africa inayosimamia vituo vya burudani vya MTV na shindano la tizo za MAMA, Bw. Monde Twala na kukubaliana kukamilisha michakato mbalimbali za kuipa Tanzania nafasi ya kuwa mwenyeji wa tuzo za MAMA kwa mwaka 2023 na kukubaliana pia uwezekano wa kuileta BET Tanzania huko mbele na kushirikiana zaidi ...
Image
  Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amekutana na kufanya mazungumzo na makamu wa Rais na meneja mkuu wa Paramount Africa and Peer Lead BET International, Monde Twala,  na kukubaliana kushirikiana katika kuiwezesha Tanzania kuwa mwenyeji wa tuzo za MAMA- MTV Africa Music Award kwa mwaka 2023. Waziri Mchengerwa amekutana na Monde Twala Jijini Los Angeles   katika jimbo la California nchini Marekani wakati wa hafla ya utoaji tuzo za BET kwa mwaka 2022. Katika mazungumzo hayo Waziri Mchengerwa amemwelezea nia na sababu ya Tanzania kutaka kuwa mwenyeji wa tamasha hilo la utoaji wa tuzo hizo kubwa za burudani kwa Afrika, kuwa ni kuongeza ushawishi kwa vijana wa kitanzania kuendelea kufanya vizuri katika sekta za burudani pamoja na kuitangaza zaidi Tanzania na uzuri wake katika ulimwengu. Katika mazungumzo hayo pande zote mbili zimekubaliana  kuungana kwenye kutafuta washirika katika kuendesha tuzo hizo, na kuridhia kuwa maandalizi yaanze ma...

Rami Tanzania mwenyeji Tuzo za (MAMA) MTV Africa Music Award 2023

Image
  Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amekutana na kufanya mazungumzo na makamu wa Rais na meneja mkuu wa Paramount Africa and Peer Lead BET International, Monde Twala,  na kukubaliana kushirikiana katika kuiwezesha Tanzania kuwa mwenyeji wa tuzo za MAMA- MTV Africa Music Award kwa mwaka 2023. Waziri Mchengerwa amekutana na Monde Twala Jijini Los Angeles   katika jimbo la California nchini Marekani wakati wa hafla ya utoaji tuzo za BET kwa mwaka 2022. Katika mazungumzo hayo Waziri Mchengerwa amemwelezea nia na sababu ya Tanzania kutaka kuwa mwenyeji wa tamasha hilo la utoaji wa tuzo hizo kubwa za burudani kwa Afrika, kuwa ni kuongeza ushawishi kwa vijana wa kitanzania kuendelea kufanya vizuri katika sekta za burudani pamoja na kuitangaza zaidi Tanzania na uzuri wake katika ulimwengu. Katika mazungumzo hayo pande zote mbili zimekubaliana  kuungana kwenye kutafuta washirika katika kuendesha tuzo hizo, na kuridhia kuwa maandalizi yaanze ma...

Tamasha kubwa la Utamaduni la mikoa yote kufanyika Dar

Image
  Na John Mapepele Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo imeanza kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan la kufanya Tamasha kubwa la kitaifa la Utamaduni ambalo linakwenda  kushirikisha zaidi ya wadau elfu ishirini. Akizungumza kwenye kikao cha maandalizi cha pamoja baina ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Saidi Yakubu amesema tamasha hilo la kihistoria linajumuisha mikoa yote ya Tanzania linatarajia kuanza Julai Mosi mwaka huu  katika uwanja wa Uhuru ambapo  maonesho mbalimbali ya  vyakula na ngoma za asili. Amefafanua kwamba Julai, 2, 2022  kutakuwa na matembezi  maalum ya kuzunguka jiji la Dar es Salaam kwenye madaraja yote  ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Kasssim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.  Kwa upande mwingine, Yakubu amesema siku ya  Julai 3, 2022...

Ubingwa wa Yanga umeleta mshikamano- Mhe Mchengerwa

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa ameipongeza timu ya Yanga kwa kutwaa kombe la katika ligi Kuu ya NBC katika msimu huu. Mhe. Mchengerwa  ameipongeza Klabu ya Yanga kwa kuchukua Ubingwa huo huku akipongeza mshikamano na furaha za mashabiki, ambazo wamezionyesha  wakati wa kukabidhiwa kombe hilo na mapokezi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. " Kwa aina ya shangwe za ubingwa zilizofanyika jana na leo ni sawa na zile za mataifa yaliyoendelea ya Ulaya. Hakika mpira wa miguu ni mchezo mkubwa na pendwa duniani ambao huwaunganisha watu pamoja na kuleta amani, mshikamano, furaha na umoja baina ya wananchi" Ameongeza kuwa watanzania zaidi ya 90% ni wapenzi wa mchezo wa soka na amesisitiza kuwa serikali itaendelea kufanya kila linalowezekana kuhakikisha inaboresha miundombinu ya michezo na kuleta usawa katika michezo hasa mpira wa miguu ili  kila mtanzania aweze kupata furaha.  "Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe...

Rais Samia aizindua MIF, aipongeza kwa kazi nzuri kwa watoto wa kike

Image
  Na John Mapepele Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan leo Juni 19, 2022 amezindua taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation (MIF) iliyopo Zanzibar inayojishughulisha na kumkwamua mtoto wa kike katika elimu ili kutimiza ndoto zake yenye kauli  mbiu inayosema “lea mwana tung’are”. Kabla ya kuzindua taasisi hiyo, Mhe. Rais Samia ameupongeza uongozi wa MIF kwa mkakati kabambe wa taasisi hiyo wa kuleta chachu ya kuunganisha Serikali na MIF na taasisi nyingine katika kumkomboa mtoto wa kike kielimu huku akielekeza serikali inavyofanya maboresho izingatie masuala ya mitaala,ukaguzi wa elimu,utungaji wa mitihani na sifa za walimu.    Aidha, Mhe. Rais ametoa wito kwa wadau mbalimbali nchini kuunga mkono jitihada zinazofanywa na MIF huku akisisitiza kuwa suala la kuwakomboa Watoto wa kike ni suala la kila mtu. “Hilo ni jukumu letu sote, tunatakiwa wote tushirikiane.” Ameongeza Mhe. Rais Amezielekeza Wizara zinahusika na elimu kwa pande zote mbili ...

Wadau wapongeza MIF kwa kusaidia mtoto wa kike Zanzibar, wajitokeza kuichangia

Image
  Na John Mapepele.  Wadau mbalimbali wa kupigania maendeleo ya mtoto wa kike nchini wamejitokeza  kuchangia takribani  shilingi  bilioni moja  kwenye  taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation (MIF) iliyopo Zanzibar inayojishughulisha na kumkwamua mtoto wa kike katika elimu ili kutimiza ndoto zake.  Wadau hao wametoa michango  hiyo katika  halfa maalum ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na taasisi ya *MIF* usiku wa kuamkia leo Juni 19, 2022 Zanzibar  kutokana na kazi kubwa na nzuri inayofanywa na mfuko huo  katika suala zima la  kuwasaidia Watoto wa kike kufikia malengo  yao hivyo kuendesha maisha yao. Mwenyekiti na Mwanzilishi wa Mfuko huo, Mhe. Wanu Hafidh Ameir ambaye pia ni Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na mtetezi wa haki  za vijana na wanawake amewashukuru wadau mbalimbali waliojitokeza ambapo amewaomba kuendelea  kuchangia ili kuwasaidia Watoto wa kike  waweze kutimiza ndoto zao. “Naom...

Mhe. Mchengerwa aipongeza Timu ya Kriketi kutwaa ubingwa Rwanda, amshukuru Rais Samia

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa ametoa pongezi kwa  Timu ya Tanzania ya  Wanawake ya Kriketi kwa  kutwaa Ubingwa leo Juni 18, 2022 kwenye mashindano ya Kwibuka Cup nchini Rwanda, yaliyoshirikisha nchi nane( Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Botswana , Nigeria, Brazil na Ujerumani) bila kufungwa na timu yoyote.  Aidha, amempongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake mkubwa anaoutoa katika michezo. Amesema hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuboresha michezo kwa kuweka mikakati  kabambe chini ya uongozi wa Samia imeleta matokeo chanya kwenye sekta za michezo na sanaa hapa nchini. Amesema taarifa ya hali ya uchumi wa nchi iliyosomwa bungeni hivi karibuni imeonesha kuwa sanaa na burudani zimechangia kwa asilimia 19.4 katika kipindi cha mwaka 2021 na kuziacha kwa  mbali sekta mbalimbali. Amesema dhamira ya Serikali kwa sasa ni kuifanya michezo kuwa uchumi badala mazoe ya kuifanya michezo kama...

Tanzania na India kuja na mapinduzi makubwa kwenye Utamaduni

Image
  Na John Mapepele. Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema  kuwa Tanzania na India zinakwenda kupitia na kuboresha mikataba ya mashirikiano ya awali  kwenye eneo la Utamaduni na Sanaa iliyojiwekea  mwaka 1984 ili  kuiboresha iweze kuleta mapinduzi makubwa na ya haraka kwa faida ya pande zote. Mhe, Mchengerwa ameyasema haya leo Juni 17, 2022 akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Hassan Abbasi wakati alipotembelewa ofisini kwake na Balozi wa India nchini Mhe.  Binaya Srikanta Pradhan na kufanya mazungumzo ya kuendeleza mashirikiano kwenye sekta hizo. Aidha, amesema mambo mengi yalikubalika   baina ya nchi zote mbili hususan  kuendelea kwa tamaduni  pia  kumekuwa na mambo mengi ambayo yameandikwa ambayo kuna haja ya kufanya mapitio. Ameongeza  kuwa katika maongezi hao  wamekubaliana kuwa  na kituo maalum cha kuandaa filamu ambacho kitatumika kwa nchi za Afrika mashariki ambapo  baa...

Southampton kuwanoa makocha wa Tanzania- Mhe, Mchengerwa

Image
  Na John Mapepele. Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema  Tanzania inakwenda  kushirikiana na klabu ya Soka ya Southampton  kuwandaa makocha wa soka ili wawe kwenye kiwango cha kimataifa. Mhe. Mchengerwa amesema haya leo juni 17, 2022 ofisini kwake akiambatana na Katibu Mkuu wa Wizara yake, Dk. Hassan Abbasi wakati alipokutana na ujumbe wa Klabu hiyo ulioongozwa na Afisa Biashara  Mkuu wa Klabu hiyo David Thomas.  Amesema dhamira ya Serikali ni kuona kuwa michezo mbalimbali inasimamiwa  kisayansi ili kuleta tija ikiwa ni pamoja na kuwa na makocha ambao watasaidia kufundisha  timu za micherzo ili kufuka kwenye kiwango cha kimataifa. Katika kikao hicho  wamekubalina kuwa Timu ya soka  ya ya Wanawake chini ya Miaka 17 (Serengeti Girls)  itakwenda kupatiwa mafunzo maalum   kwenye Klabu hiyo ikiwa ni maandalizi ya kwenda kwenye  mashindano ya kombe la dunia nchini India. Katika tukio hilo ...

Kiongozi Mabohora Duniani Atua kufanya “Royal Tour” Tanzania

Image
   Kiongozi Mkuu wa madhehebu ya Kiislamu ya Mabohora (Dawoodi Bohoras); Sheikh Syedna Mufaddal Saifuddin, ametua nchini leo Alhamisi Juni 16, 2022, tayari kufanya ziara ya kiimani na mapumziko mafupi.  Saydna Mufaddal, atakuwa nchini kwa takribani wiki mbili ambapo pamoja na shughuli za kiimani amekuja kuunga mkono azma ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuitangaza na kuifungua nchi hasa kupitia filamu ya Royal Tour. “Akiwa nchini amekuja kuunga mkono malengo ya Royal Tour na yeye mwenyewe na wafuasi wake watakwenda mapumziko hapa nchini na msafara wake wote katika maeneo mbalimbali na pia iwapo taratibu zitakamilika na akaridhia anaweza kufanya mhadhara wake mkubwa wa kidini Julai hapa nchini ambapo wafuasi wake kati ya 30,000 hadi 40,000 kutoka sehemu mbalimbali duniani humfuata na tunajipanga ikitokea hivyo tutawaonesha watu hao na mabohora wengine duniani filamu ya Royal Tour,” alisema mmoja wa viongozi wa dhehebu hilo nchini Bw. Zainuldeen Adamjee.  Akimpokea Kiong...