SERIKALI KUENDELEA KUZIPATIA UFUMBUZI CHANGAMOTO ZA MUUNGANO
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakiwa wamesimama kwa dakika moja kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati ikiwa ni ishara ya kumkumbuka aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magulifuli. Kamati hiyo imekutana hii leo Machi 28, 2021 katika Ukumbi wa Msekwa jijini Dodoma kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa fedha 2020/2021 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2021/2022. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa fedha 2020/2021 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2021/2022 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria hii leo Machi 28, 2021 katika Ukumbi wa Msekwa jijini Dodoma. Meza kuu ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Mohamed Mchengerwa (katikati) Makamu Mwenyekiti Mhe. Najma Giga na Katibu wa Kamati ...